Kampuni ya simu nchini, Vodacom Tanzania ikishirikiana na Huawei, wamezindua smartphone kali, Kishkwambi kwa lengo la kuhakikisha watanzania wanapata haki yao ya mawasiliano na kumiliki sio simu tu bali simu ya kisasa.

Meneja wa Huawei nchini Tanzania Huxiangyang Jacko akitoa hotuba kwenye mkutano na waandishi wa habari katika uzinduzi simu mpya ya Huawei kishkwambi inayokuja na ofa kabambe kutoka Vodacom. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na usambazaji Vodacom Tanzania George Rwehumbiza na Mkurugenzi wa mauzo na Usambazaji wa Huawei Tanzania Bwana Sylvester Manyara
Huawei imeshirikiana na Vodacom Tanzania kuleta simu ya Huawei Kishkwambi iliyounganishwa na kifurushi cha Vodacom cha muda wa maongezi na internet.
Promosheni ya Huawei Kishkwambi inaenda sambamba na uzinduzi wa maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Saba Saba. Simu hii inanunuliwa kwa shilingi 100,000 tu, ikiwa na kifurushi cha bure cha internet cha GB6 na dakika 100 za bure za maongezi katika mtandao wa 3G wa Vodacom kwa mwaka mmoja. Simu hii pia huja na waranti ya miezi 12 kutoka Huawei.
Mkurugenzi Mkazi wa Huawei Huxiangyang Jacko anasema, “Huawei imedhamiria kufikia maeneo yote ya soko la Tanzania kupitia bidhaa zao nyingi ambazo pia zimethibitika kufanya vema katika masoko mengine ulimwenguni. Lakini kwa Tanzania, tunataka kuweka mkazo kwa watu wa kipato cha kati na cha chini, wanafunzi na wafanyakazi vijana ambao wanathamini ubora na pia wanajali bei. Kwa sababu hiyo, Huawei Kishkwambi inaonesha kuwa ndio simu bora tunayoweza kuwapatia wateja wetu ambayo yaweza kuwa ndio simu ya kwanza au pia kwa wale wanaotaka kuongeza simu ya pili.”.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza alisema ushirikiano wao na Huawei unaendana na nia ya Vodacom Tanzania ya kuwapatia wateja wao fursa ya kununua simu bora na za bei nafuu hususani baada ya zoezi la hivi karibuni la uzimaji simu feki lililotekelezwa na TCRA.

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na usambazaji Vodacom Tanzania George Rwehumbiza akitoa hotuba kwenye mkutano na waandishi wa habari katika uzinduzi simu mpya ya Huawei kishkwambi inayokuja na ofa kabambe kutoka Vodacom
“Vodacom Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wateja wake wanaendelea kuunganishwa hata baada ya uzimaji mkubwa wa simu uliofanywa na TCRA, hivyo basi ushirikiano wetu na Huawei unaongeza msukumo wetu kuhakikisha kuwa wateja wetu wanabakia wakiwa wameunganishwa na katika hilo pia tunawapatia motisha ya vifurushi vya internet na muda wa maongezi lukuki” alisema afisa huyo wa Vodacom Tanzania.
Huawei Kishkwambi ni simu iliyowezeshwa kwa 3G na inazo sifa zote za simu za kisasa, na kwa vifurushi vya gharama nafuu vya muda wa maongezi na internet wateja wanaweza kuperuzi mtandaoni, Facebook na hata Instagram. Simu hii ina kioo cha LCD cha inchi 4. Ili kuleta mvuto wa kipekee, Huawei Kishkwambi ina mgongo wenye mkunjo kwa mbali na kona zake nne zilizopinda bila ncha kali. Muundo wake huu wa kipekee unawapa watumiaji wake hisia nzuri wanapoishika na ni rahisi kuitumia hata kwa mkono mmoja.
Ina megapikseli 0.3 katika kamera yake ya mbele na megapikseli 2 katika kamera ya nyuma. Huawei Kishkwambi ina prosesa 2 ambazo huipa uwezo wa kufanya kazi haraka sana katika kucheza michezo ya kwenye simu (game). Kadi yake ina ukubwa wa MB512 na ROM ya GB4 ambayo inaweza kuongezwa kwa kadi ya nje. Simu hii ina spidi ya hali ya juu na uwezo mkubwa wa kutunza chaji.
Ushirikiano huu wa kipekee wa miamba miwili ya kimataifa nchini Tanzania ni hatua ya kimkakati ya Huawei na Vodacom ya pamoja katika kuleta suluhisho kwa watumiaji wa simu. Kila simu ya kisasa inahitaji kuunganishwa na mtandao bora ili kuleta ubora halisi kwa mtumiaji wa simu. Hapa ndipo utendaji wa simu ya Huawei Kishkwambi unapoendana na mtandao wenye kasi wa Vodacom 3G kuleta nguvu Zaidi kwa watumiaji.

Kutoka kushoto ni Meneja wa Huawei nchini Tanzania Huxiangyang Jacko akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na usambazaji Vodacom Tanzania George Rwehumbiza, Mkurugenzi wa mauzo na Usambazaji wa Huawei Tanzania Sylvester Manyara na mwisho ni Edwin Byampanju meneja bidhaa kutoka Vodacom wakionyesha kipeperush cha simu mpya ya Huawei kishkwambi wakiwa mara baada ya mkutano na waandishi wa habari katika uzinduzi wa simu hiyo inayokuja na ofa kabambe kutoka Vodacom, uliofanyika katika ukumbi wa Western Coral Beach Hotel, jijini Dar es Salaam
Katika kufanikisha wazo la serikali kuwa haki ya kuwasiliana inapaswa kumfikia kila mtanzania, Vodacom imekuwa ikifanya jitihada pasipo kuchoka katika kuwaunganisha watanzania na kuongeza uwekezaji katika sekta ya mawasiliano ya simu. Ushirikiano na Huawei katika promosheni ya Huawei Kishkwambi ni moja ya namna nyingi ya ofa zinazotolewa kwa wateja. Promosheni hii maalum ya Huawei Kishkwambi inatolewa katika maduka yote ya Huawei na Vodacom nchini kote. Huawei na Vodacom kwa pamoja zinawahimiza watanzania kuitumia vilivyo fursa ya promosheni hii na kufurahia kuendelea kuunganishwa kimawasiliano.
0 maoni:
Chapisha Maoni