mdudu

mdudu

WARCH ONLINE NEW VIDEO

SIKILIZA NA DOWNLOAD NGOMA KALI MPYA

Ijumaa, 1 Julai 2016

Young Dee akirekebisha makosa aliyofanya Mtu Chee ruksa kurudi kundini – Stamina



Kwa mujibu wa Stamina kuondoka kwa Young Dee kwenye kundi la Mtu Chee kulitokana na kupishana kauli kati yake na Country Boy, na kwamba kama atarekebisha makosa aliyowafanyia wako radhi kumrejesha kundini.
13531968_1101664066571243_1094846367_n
Hivi karibuni Young Dee alithibitisha tetesi za kutumia madawa ya kulevya na kutangaza kuwa ameacha. Wiki hii ameachia ngoma yake mpya ‘Hands Up.’
“Kulikuwa na misunderstanding baina yake yeye na Country Boy,” Stamina alimweleza mtangazaji wa Jembe FM, JJ.
“Anytime kama ataona yeye ndio alikosea kama alivyorekebisha mistakes zake katika management yake, kama ataweza kurekebisha mistakes zake pia kwenye kundi anakaribishwa anytime hakuna mtu mwenye bifu naye ni mambo tu ya kikazi na kipindi cha kati alipokuwa amechanganyikiwa na madude yake hayo kwahiyo ndio maana ilikuwa ni ngumu kuweka kukaa chini na kusolve chochote,” aliongeza.
“Lakini sasa hivi kama yupo competent kabisa anaona anaweza kusolve chochote anakaribishwa muda wote.”
Miezi kadhaa iliyopita Mtu Chee waliachia ngoma bila Young Dee na kumshirikisha Young Killer.

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Online Project management