Wakala kupambana na wafunga lumbesa
Hatua hiyo inatokana na kuwa faini wanazotozwa ni ndogo kiasi ambacho hawaoni athari ya ukiukwaji huo wa sheria na vipimo wanaofanya, hivyo kwa kupelekwa jela wataona uchungu na kuachana na ufungashaji huo.
Ofisa Habari wa wakala huo, Paulus Oluoch alisema kuwa sheria iliyopo ni ya zamani ambayo ni sheria ya vipimo sura namba 340 na mapitio yake ya mwaka 2002, imepitwa na wakati.
Alisema katika sheria hiyo inaainisha kuwa mtu akikutwa na kesi ya kufungasha mizigo kwa mtindo wa lumbesa kama ni kosa la mara ya kwanza anatakiwa kulipa faini ya Sh 10,000 au kifungo cha miaka mitatu au vyote kwa pamoja.
Pia sheria hiyo inaeleza kuwa iwapo atarudia kosa hilo kwa mara nyingine basi atatozwa faini ya Sh 20,000 au kifungo cha miaka saba jela au vyote kwa pamoja, hivyo kwa faini hizo hawasikii uchungu kwa kosa walilofanya.
Oluochi alisema kwa sasa wanaendelea na operesheni nchi nzima kuangalia ufungashaji huo wa lumbesa huku wakitoa elimu kwa wakulima kuhusu matumizi ya mizani ya kupimia mazao na kuwapa njia zitakazowasaidia kuepuka kuibiwa.
“Wafanyabiashara wanaonunua mazao wana njia tofauti ambazo wakulima wanaibiwa ikiwa ni pamoja na kuhesabu kilo wenyewe wakulima wakiwa wamekaa mbali na mizani, huku mizani mingine wakiwa wameichezea na kuiba kila mzigo baadhi ya kilo,”alisisitiza.
0 maoni:
Chapisha Maoni