mdudu

mdudu

WARCH ONLINE NEW VIDEO

SIKILIZA NA DOWNLOAD NGOMA KALI MPYA

Jumapili, 3 Julai 2016

CHUO KIKUU DAR CHAZALISHA PEREGE DUME

Chuo Kikuu Dar chazalisha perege madume

TAASISI ya Sayansi za Bahari(IMS)ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, imefanya utafiti wa samaki na kufanikiwa kuzalisha samaki aina ya perege madume wa asili wasiozalishwa kwa kutumia teknolojia ya kubadilisha kinasaba(GMO), hivyo kuwa aina ya kwanza ya samaki hao duniani kuzalishwa Tanzania.
Akizungumza kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam, Mhadhiri Mwandamizi wa IMS, Dk Avit Mmochi alisema hayo ni mafanikio makubwa kwa taasisi hiyo.
Alisema tangu mwaka 1996 taasisi hiyo ilianza kufanya utafiti wa samaki wa baharini na ilipofika mwaka 2004 walifanikiwa kuzalisha aina mbalimbali za samaki wanaoweza kufugwa kwenye maji mchanyanyiko na wakakua bila matatizo.
Dk Mmochi alisema mwaka 2015, IMS ilianza kufanya utafiti wa kuzalisha samaki aina ya perege madume na kufanikiwa kuyazalisha bila kutumia teknolojia ya kinasaba, hivyo kuwa nchi ya kwanza duniani kuzalisha aina hiyo ya samaki wasiotumia dawa za kiteknolojia.
Alisema katika utafiti huo walitumia madume ya samaki waitwao Rufiji kutoka eneo la Rufiji ambao wanastahmili maji chumvi, wanawachanganya na majike ya samaki aina ya Sato kutoka Ziwa Victoria na wakafanikiwa kuzalisha madume matupu ya perege hao.
Alisema Ufilipino wapo samaki kama hao lakini tofauti na hawa wa Tanzani ni kwamba wao wa Ufilipino wamewazalisha kwa kutumia teknolojia ya GMO, ambayo inatumia dawa zinazoweza kuwa na madhara kwa watumiaji.

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Online Project management